Juma Nature bado ameendelea kudhihirisha ule usemi wa mtaani kuwa 'ana kizizi' baada ya kupata 'zali la mentali' la kupafomu wimbo mmoja na msanii kutoka Marekani Lil Kim kwa kumpelekesha katika wimbo wake wa Mugambo ambao ulichengua maelfu ya mashabiki waliofurika katika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia leo. Nature alikuwa msanii pekee aliyepata bahati ya kuimba jukwaa moja na msanii huyo ambaye alionekana kumzimia ile mbaya kwa kum' hagi na kumpiga mabusu mara kwa mara hadi kupachikwa jina la Shemeji!.
No comments:
Post a Comment