Friday, August 13, 2010

Miss Universe Bongo ‘kutifuana’ na wazungu


Hellen Dausen.




Mrembo wa Tanzania ambaye anatuwakilisha katika Shindano la Miss Universe Dunia mwaka huu, Hellen Dausen anatarajia kutifuana na washiriki wengine kutoka nchi mbalimbali Agosti 23, mwaka huu.



Habari kutoka mtandaoni mrembo huyo pamoja na wengine kwasasa wako katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuingia katika mtanange wa kuliwania taji analolishikilia mwanadada Stefania Fernandez raia wa Venezuela ambaye ndiye Miss Universe 2009.

Mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la Miss Universe World 2010, Hellen Dausen (kulia) akiwa na washiriki wenzake nchini Marekani hivi karibuni.




“Warembo wako katika Hoteli ya Mandalay Bay iliyopo Las Vegas, Marekani kujiandaa na shindano hilo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.



Shindano hilo linatarajiwa kuoneshwa laivu na Kituo cha Televisheni cha NBC huku wasanii kama vile Bret Michael, John Legend & Kundi la ‘The Roots’ wakitarajiwa kulisindikiza.

No comments:

Post a Comment