Monday, August 9, 2010

TIP TOP CONNECTION.


Kundi la Muziki wa Kizazi Kipya la Tip Top Connection




Na Mwandishi Wetu

Kundi la Muziki wa Kizazi Kipya la Tip Top Connection, lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, lilitia fora kwenye Tamasha la Fiesta mwaka huu kwa staili ya mavazi waliyopanda nayo jukwaani.



Wakati wakali hao wakipanda jukwaani usiku wa kuamkia jana katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, walionekana nadhifu kinoma kutokana na kupiga suti za ukweli.



“Duh! Washkaji noma hawa, cheki wote wamevunja kabati, mwendo wa suti na tai, usipime...” alisikika shabiki mmoja akisema.



Wakati wasanii wa kiume wakiwa wamepiga suti, Keisha alikwenda kwa mwendo wa suruali na blauzi ambazo zote zilimsitiri vyema na hivyo kuonekana ndiyo wasanii pekee waliovalia nadhifu zaidi

No comments:

Post a Comment