Tuesday, August 10, 2010

Wanawake wanavyosababisha upungufu wa nguvu za kiume .

Nashukuru tangu tulipoanza somo hili wiki iliyopita wanaume wengi wamekiri kupungukiwa nguvu za kiume, na walikubaliana na maelezo niliyotoa katika sehemu ya kwanza ya mada hii. Leo naomba tumalizie sehemu ya pili na ya mwisho ya mada hii, kwa kuanzia pale tulipoishia.




1: KAULI

Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.



Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”



2 : UJUZI

Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.



Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo.

Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.



Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.



USAFI

Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi ni muhimu sana katika mapenzi.

Itaendelea wiki ijayo...

No comments:

Post a Comment