Thursday, August 12, 2010

TATIANA:SIJUTII...

Mshiriki wa Big Brother Africa ‘All Stars’ 2010, Tatiana Durao ‘Tati’ (29), ameibuka na kudai kuwa, hajutii kutembea na mume wa mtu ndani ya BBA kwani alikuwa na uwezo wa kutembea na mwanaume yeyote yule lakini kwa jamaa mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Richard alikuwa amefika.




Tati aliyasema hao mwanzoni mwa wiki hii alipokuwa akigonga stori na mshiriki mwenzie kutoka Zambia, Paloma ambaye alimwambia kuwa hakutakiwa kutembea na Richard kwa sababu alijua wazi ni mume wa mtu.



“Haukua sahihi hata kidogo ‘bebi’ kwa sababu mwanaume huyo hakuwa mali yako,” alisema Paloma huku Tati alipojaribu kujitetea kwa kusisitiza kuwa alimweleza kwakuwa ni rafiki yake na urafiki wa kweli ni kuambiana.



Tati alimalizia kwa kudai kwamba, kwa sasa hawezi kurudia kuwa na mwanaume kama ilivyokuwa mwaka juzi kwani amekua mwanamke mkubwa.

No comments:

Post a Comment